Fahamu Fedha za Umma
Mapato
Mapato yanatoka wapi?
Serikali hupata fedha kutoka kodi, tozo, ruzuku na mikopo.
Mambo muhimu
- Kodi ndiyo chanzo kikuu cha mapato ya taifa.
- Halmashauri hukusanya ushuru na ada zake.
- Ruzuku na mikopo hujaza pengo linalobaki.
Kila unaponunua bidhaa au kulipa ushuru wa soko, unachangia mapato ya umma. Kwa hiyo fedha za umma ni fedha zako.
Kujua kiasi kilichokusanywa katika halmashauri yako hukusaidia kuuliza kimetumikaje.