Kuhusu Mradi
Wajibika Kidigitali unaimarisha uwazi, uwajibikaji wa fedha za umma na ushiriki wa wananchi.
Wajibika Kidigitali ni mradi wa Policy Forum kwa kushirikiana na WAJIBU – Institute of Public Accountability, unaofadhiliwa na Ubalozi wa Kifalme wa Norway jijini Dar es Salaam. Mradi unatekelezwa kuanzia Julai 2026 hadi Novemba 2027.
Mradi unalenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji wa fedha za umma na ushiriki wa wananchi, hasa katika mikoa ya Morogoro na Mtwara.
Mradi unatumia zana za kidijitali, zikiwemo akili bandia, chatbot, kituo cha taarifa cha kidijitali na USSD, ili taarifa za fedha za umma ziwafikie wananchi kwa lugha rahisi.